Rais Samia ameteua mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amemteua Prof. Wineaster Saria Anderson kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE). Prof. Anderson anachukua nafasi ya Prof. Eleuther Mwageni ambaye alifariki mwezi Julai, 2021. Uteuzi huo umeanza tarehe 07 Novemba, 2021.